Thursday, October 17, 2013

TANZANIA IMESHUKA VIWANGO FIFA HUKU UGANDA IKIONGOZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Tanzania imeshuka tena kwa nafasi mbili katika chati ya viwango vya ubora wa soka duniani kutoka 127 hadi 129, kwa mujibu wa
orodha mpya iliyotolewa jana na shirikisho la soka la kimataifa (FIFA).


Uganda imeendelea kuongoza ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikishika nafasi ya 85 licha ya kuanguka kwa nafasi nne kutoka 81 iliyokuwapo mwezi uliopita.

Katika ukanda huu, Uganda inafuatiwa na Ethiopia iliyo katika nafasi ya 95 duniani, Kenya (118 duniani), Burundi (121), Rwanda inafungana na tanzania katika nafasi ya 129, Sudan (136), Eritrea (195), Somali (201), Djibout (202) na Sudan Kusini (204). 

0 comments:

Post a Comment