Tuesday, October 29, 2013

ROMA MKATOLIKI KUTOKA KIVINGINE IJUMAA HII

Msanii mkali wa Hip Hop Tanzania anayewakirisha vilivyo mkoa wa Tanga mwite Roma Mkatoliki ambaye mpaka sasa anatamba na Ngoma yake ya 2030
ameamuwa kuvunja ukimya kwa kuachia Video yake ya Kwanza Toka alipoanza Game.
Roma Mkatoliki ambaye anatoa wimbo mmoja kwa mwaka mzima amedai kuwa Video yake ya Kwanza itakuwa ni 2030 ambayo ndiyo itatambulishwa rasmi kwa Wananchi siku ya Ijumaa hii,2030 imefanywa na Director ambaye kwa sasa amelenga kufanya mapinduzi katika Tasnia ya Production Bongo hususani katika Muziki kwa kufanya Vichupa Vikali.

Nisher ndiye aliyetengeneza Video ya Jikubali ya Ben Paul pamoja na Kijukuu ya Young D na nyingine nyingi ambazo zimefanya poa kunako Tasnia ya muziki Bongo.

0 comments:

Post a Comment