NGE-SCORPIO OKT 23-NOV 22:
Mchana
huu ni mbaya kwako katika masuala ya kazi au pesa, kuwa mwangalifu na
mambo yanayokuhusu, kwani kuyapuuza kunaweza kukupeleka pabaya.
Jaribu kuzungumza na watu wako wa karibu
wakusaidie.
MSHALE-SAGITTARIUS NOV. 23-DES 20:
Mchana huu
safari yeyote utakayoifanya leo itakuwa ya hasara kubwa, ni bora
safari hiyo uifanye kwa kuwatembelea wakubwa wako wa kazi Jitahidi
wiki hii usigombane na mtu yoyote utapata matatizo.
MBUZI-CAPRICON
DES 21-JAN 18: Mchana huu katika ndoto utakazoota kuna zile ambazo
zitakuwa zinakuelewesha namna ya kuongeza kipato chako. Jaribu
kuzikumbuka na uzitekeleze kadri ulivyoota, utapata
faida.
NDOO-AQUARIUS JAN 19-FEB 18:
Mchana huu jihusushe
sana na shughuli yeyote ile hata kama si yako, kwa sababu nyota
zinaonyesha kwamba kutojihusisha kwako katika mambo ya biashara
kutakufanya ukose kabisa kutekeleza malengo yako.
SAMAKI-PISCES
FEB 19-MACH 20:
Mchana huu jitahidi kujithibiti na kukasirika kwa
sababu hasira zako zitakupeleka pabaya, mambo ya Polisi na Kesi
yatakuandama. Jaribu kuweka akiba kuna matatizo mbele
yako.
PUNDA-ARIES MACH 21-APR 20:
Mchana huu ni mbaya
kwani mambo yako mengi yatavurugika, unashauriwa kuanzisha biashara
mpya ili kujiongezea kipato chako, miradi yako ulionayo unatakiwa
kuiboresha zaidi usiiache.
NG’OMBE-TAURUS APR 21-MEI20:
Mchana huu ni nzuri kwako, kwani utapata mpenzi mpya
atakayekuongoza katika mafanikio ya kimaisha. Mpenzi wako wa zamani
usimuache haraka kwa sababu kuna wasiwasi wa yeye kukufanyia uchawi.
Fanya mambo kwa utaratibu.
MAPACHA-GEMINI MEI 21 - JUNI 20:
Mchana huu ni nzuri kwako, katika shughuli zako za kikazi na
kijamii, ugomvi ulionao kati yako na mpenzi wako utakwisha, Jaribu
kuwa mvumilivu katika masuala ya mapenzi au utakosa maisha.
KAA-CANCER JUNI 21-JULAI 20:
Mchana huu ni siku mbaya
kwako katika masuala ya pesa au katika mahusiano na watu. Kuna
matatizo ya ugomvi yatakayokufanya ukamatwe au ulale ndani. Jiepushe
kabisa na marafiki wabaya watakupeleka pabaya.
SIMBA-LEO JULAI
21-AGOSTI 21: Mchana huu ni nzuri kwako kukutana na wakubwa wako wa
kazi kuhusiana na mambo yako, Jaribu kuwa na unyenyekevu ili uweze
kutatuliwa tatizo lako. Ni vizuri kuwa makini katika kila jambo hasa
la kazi.
MASHUKE-VIRGO
AGOSTI 22-SEPT 22:
Mchana huu unatakiwa ufanye kazi kwa bidii
sana, kuna maneno ambayo bosi wako ameambiwa yanaweza kukukosesha
kazi. Jichunge sana na msaidizi wako atakuumiza.
MIZANI-LIBRA
SEPT 23-OKT 22:
Mchana huu utapata bahati ya fedha, uwe makini
nazo, kwani kuna watu wengine watajifanya kukuangukia na kuwa wema
kwako, yote hayo ni kutaka kukupotezea malengo na kula fedha zako.
Usiwakubalie.







0 comments:
Post a Comment