Kiungo
wa Yanga Mnyaruanda Haruna Niyonzima amepata majanga baada ya nyumba
anayoishi kuungua kwa moto
usiku wa kuamkia leo maeneo ya Magomeni
Makuti Dar es salaam.
Kutokana
na kuungua kwa nyumba hiyo iliyokuwa na wapangaji wawili imesababisha
hasara na uhalibifu wa vitu mbalimbali hasa zaidi katika Furniture na
vitu vya sebuleni vikiwemo Luninga,Radio na vitu vingine
vilivyotumika kupamba sebule ya Mchezaji huyo wa Yanga.
Wakati
nyumba hiyo ikiwa inateketea kwa moto Haruna Nyionzima alikuwepo
ndani ya nyumba hiyo na kusaidiwa na majirani katika kuzima moto huo.







0 comments:
Post a Comment