Wednesday, October 30, 2013

MCHEZAJI WA COASTAL ANAYEJIVUNIA KUTOKA MBEYA.

Kwa jina anafahamika kama Uhuru Seleman ambaye safari yake ya katika Soka ilianza miaka ya 90s akiwa Mkoani Mbeya katika Wilaya ya Mbarali akiwa
anacheza soka katika Timu ya shule.
 
Kwa kupenda kazi yake ya mpira alianza kuonesha mbwembwe na kufanikiwa kufanya vizuri katika maisha ya soka toka akiwa na umri mdogo kwa kuwakimbiza na kuonesha kiwango kizuri cha soka.

Daima mtafutaji huwa hachoki na kama akichoka basi huwa anakuwa ameshapata,harakati zake za kutafuta mpira bora na wa mfano hazikuisha wala hakukatishwa tamaa alianza kusajiliwa katika Timu mbalimbali akiwa bado yupo nyanda za juu kusini ambapo alishawahi kuchezea Timu ya Wilaya Mbarali mara kadhaa,kwa kuwa uwezo wake ulimruhusu kupenya alifanikiwa kuonekana katika Soka na kusonga mbele mpaka Mafinga mkoni Iringa ambapo mbali na kazi mbgalimbali alizokuwa akifanya alipiga soka.

Kujituma na Uwezo wake ulizidi kuonekana zaidi maana siku zote king'aacho huna kinaonekana na watu wengi sana hapo ndipo alipoanza kufunguka kwa kasi kubwa mpaka wadau wa soka Tanzania kumuelewa Mwambungu ni nani.

Tukiachia Safari yake ya Soka aliyoanza muda mrefu pasipo kuwa na mafanikio makubwa lakini alizidi kuonesha uwezo na kupasua anga.

Mafanikio makubwa kisoka kwa Uhuru Selleman yalianza pale alipokuwa katika Kikosi cha Mtibwa Sugar kwani hapo ndipo Watanzania waliona uwepo wake katika Soka na kufanikiwa kufika katika Timu Kubwa zilizo na ushindani nazungumzia Simba Sports Club,na hapo ndipo alipata nafasi ya kuichezea Azam Fc na Timu ya Taifa Stars.

Lakini kwa sasa Mkali huyo anapatikana katika Kikosi cha Coastal Union kilicho na makazi yake mjini Tanga lakini anaamini mafanikio yake katika Soka yametokana na mapenzi ya kweli ya watu wa mbeya ambao kwa namna moja au nyingine walikuwa wakimfaliji kwa kile alichokuwa akikifanya.
Najivunia kuzaliwa mbeya Najivunia kutokea mkoa wenye mashabiki wanaopenda vya nyumbani kama hawa naipenda mbeya naupenda mpira nawapenda mashabiki wote wa mbeya GET UP GREEN CITY”



0 comments:

Post a Comment