Friday, October 18, 2013

MANENO MACHACHE KUTOKA TIMU YA MBEYA CITY

Ndugu mashabiki wa Mbeya City na watanzania kwa ujumla wetu, Timu yenu kesho inashuka dimbani tena dhidi ya Timu ngumu ya Ruvu JKT, katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Mbeya hivyo basi vijana
wenu wanaomba ushirikiano wenu wa maombi na shangwe uwanjani, ili kuwatia moyo katika harakati ya kuzinyakua pointi Tatu muhimu kesho. Tiketi zitauzwa shilingi elfu Tatu 3,000 tu.

kuanzia saa nne Asubuhi kesho katika vituo vifuatavyo. Sokoine uwanjani, Mwanjelwa, Kabwe, Pamoja na Uyole. wachezaji wapo katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo.

0 comments:

Post a Comment