Mkali wa Bongo Fleva
ambaye kwa sasa ametambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la
Bashasha aliyempa shavu Vanesa amesema kuwa ameachana na Mkewe ambaye
amezaa naye mtoto mmoja wa Kiume.
Msanii Bob Junior
akifunguka kupitia Kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio
amesema kuwa ameachana na mkewe kwa sababu ya wivu wa Mapenzi
aliyokuwa nao huyo ambaye alikuwa mkewe ambaye ameweza kumzawadia Bob
Junior Mtoto Mmoja wa Kiume.
Bob Junior amefunguka
na kusema kuwa wale wote waliosema kuwa alioa ili aweze kupikiwa
kipindi cha mfungo si kweli bali wameshindwana na mkewe kwa sababu za
Kifamilia na Wivu wa Mapenzi,lakini mkali huyo hajaishia hapo bali
amekaribisha Maombi kwa yoyote ambaye atakuwa tayari bali anapaswa
kuwa na Tabia njema tu.







0 comments:
Post a Comment