Aliyekuwa
Daktari Binafsi wa Mfalme wa Pop Duniani Michael Jackson ambaye
alituhumiwa kusababisha kifo cha Mwanamuziki huyo na kufungwa kifungo
cha miaka Minne gerezani amechiwa huru leo.
Conrad
Murray alituhumiwa kifungo cha miaka Minne Gerezani baada ya kukutwa
na hatia ya kusababisha kifo cha Michael Jackson kwa kumdunga Dawa
zilizopeleke Kifo cha Jackson .
Ikiwa
Miaka Miwili imeshapita toka kukutwa na Hatia ya kuuwa pasipo
kukusudia leo ameachiliwa huru baada ya kutumikia kifungo hicho
zaidi ya miaka miwili toka alipohukumiwa November 2011 .
Taarifa
za Gereza alililokuwa amefungwa Murrays zimethibitisha Kutolewa kwa
Daktari huyo hata afisa wa Gereza pia amethibitisha kuwa ameachiwa
muda 12:01 Jumatatu.
Michael
Jackson alikufa siku ya Tarehe 25 June 2009 baada ya kuzidishiwa dozi
na Daktari Murray.
Murray
ambaye kwa sasa ana umri wa Miaka 60 alifungwa miaka Minne lakini
kubadilika kwa Sheria za California kumepelekea kupunguza kwa vikwazo
kwake







0 comments:
Post a Comment