Monday, October 28, 2013

BATURI AWAPONDA WASANII WANAOJIPODOA MISIBANI

Msanii katika Kiwanda cha Filamu Nchini Tanzania Baturi amefunguka na kutoa ya moyoni kwa Wasanii na Raia wengine ambao kazi yao ni kujiremba na
kujipodoa Pindi waendapo katika Misaba,kwani amefananisha hali hiyo ni sawa na Kwenda kuuza Sura wakati wenzako wapo katika Kipindi Kigumu.
 
Katika Hali isiyo ya Kawaida kumekuwa na Tabia ya Muundo huu wa Watu wengi katika Kizazi cha sasa kutinga katika maeneo ya misiba  kama wanakwenda hudhuria sherehe au kama wanakwenda katika Vikao vya Dili kutokana na jinsi wanavyokuwa wamejiweka hasa kimavazi,na upande wa kina dada ni kama wanakwenda katika Maonyesho ya Mavazi au vitu vya Dhamani wanavyomiliki.

0 comments:

Post a Comment