Friday, September 6, 2013

UONGOZI WA YANGA UMESEMA MWALUSAKO BADO NI KAIMU KATIBU MKUU YANGA

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Clement Sanga leo amefanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kutoa ufafanuzi juu ya kuondolewa kwa Kaimu Katibu Mkuu..!
wa Club hiyo Lawrence Mwalusako,Mwenyekiti huyo amesema kuwa hakuna mabadiliko yoyote yale na Kaimu Katibu Mkuu Lawrence Mwalusako ataendelea kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga mpaka hapo Tarrifa nyingine itakapotolewa.
 
Napenda kutoa taarifa kwa umma na wanachama wa Yanga kuwa uongozi bado haujatoa baraka za ajira kwa mtu yoyote katika nafasi hizo, isipokuwa muombaji Patrick Naggi aliwahi kufika makao makuu ya Klabu kabla ya mchakatao wa usahili kukamilika.

Lawrence Mwalusako anaendelea kuwa kaimu katibu mkuu wa Yanga mpaka hapo kutakapokuwa na taarifa nyingine zozote za mabadiliko kwa nafasi zote zilizopo wazi katika idara mbalimbali.

Uongozi unawaaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa soka kuwa kitu kimoja katika kuunga mkono harakati za kimaendeleo ili kuifanya timu iende katika hatua nyingine ya ushindani wa kimatifa. 



0 comments:

Post a Comment