Tuesday, August 13, 2013

ZITTO KABWE AZITAKA MAMLAKA ZINAZOENDESHA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA KUWAJIBISHWA KWANI HAKUNA ZIKIFANYACHO.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Zuberi Kabwe jana katika Kikao cha kamati za Bunge kilichofanyika mjini Bagamoyo amezitaka Mamlaka zinazoendesha Vita dhidi ya Madwa ya kulevya.....!kuwajibishwa kwani hakuna walitendalo.
Zitto alisema kauli hiyo kutokana na ukweli kwamba kila mwaka kuna fungu linatengwa likiwa na lengo la kupambana na biashara halamu ya madawa ya kulevya lakini cha ajabu kila siku inapokwenda biashara hii ya madawa ya kulevya inazidi kuota mizizi na kushamili kwa kasi kubwa Nchini.
" sasa nchi yetu imekuwa kitovu cha biashara ya dawa za kulevya. Vijana wa kitanzania wamekuwa wakikamatwa maeneo mbalimbali duniani wakihusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. Moja ya njia ya kupambana na uharamia huu ni uwajibikaji wa mamlaka zenye wajibu wa kupambana na madawa ya kulevya”
Pia Zitto alizitaka Kamati za Bunge kuhoji matumizi na mahesabu ya mamlaka hizo ambazo zinapata fedha za umma katika kupigana vita dhidi ya madawa ya kulevya wakati biashara hizo zinazidi kushamili na kuota mizizi Nchini.
Hatuwezi kuwa tunatenga fedha kila mwaka dhidi ya biashara hii haramu lakini bado inazidi kushamiri. Kila mwenye wajibu awajibishwe"

0 comments:

Post a Comment