Tuesday, August 13, 2013

NYOTA YAKO LEO JUMANNE: 13/8/2013

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Pamoja na juhudi kubwa unayofanya kazi zako zitakwenda polepole, kukata tamaa liwe jambo la mwisho kwa upande wako...!



MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Masuala ya mapenzi yatakuwa na wakati mzuri sana hasa siku ya leo,ile furaha iliyopotea sasa inaweza kurudi na kukuweka kwenye matumaini makubwa.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Unahitaji muda mwingi zaidi kabla ya kufanya maamuzi kwa mambo yaliyo mbele yako, ushauri si lazima kama unajiamaini.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Kama utashindwa kuwa karibu na watu wanaokutegemea basi waonyeshe njia ya wao kuweza kujisaidia, kwa kufanya hivyo utakuwa umejikomboa.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 23)
Ni wakati wa kuwafungulia milango watu wapya, mafanikio yako yataendele kukusogeza karibu na watu wengi.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20
Jiweke mbali na migogoro na wala usishiriki kwenye maamuzi yatakayoonyesha kuwa na mashaka kwa upande wako.

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 19)
Nguvu kubwa unayotumia katika kazi zako inaonekana kupungua, ni wakati wa kufanya mabadiliko sasa.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Nafasi za kufanikiwa ziko mbel yako, jitihada zako ndizo zinaweza kuamua wapi unaweza kufanikisha ndoto zako.

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Mawazo yako yanakupeleka mbali lakini hata hivyo unahitaji kujituma zaidi na kuwashirikisha watu wengine katika maamuzi.

NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Kauli zako zinaweza kuwa na maana isiyoeleweka mbele ya wengine kwa kuepuka matatizo, kuwa makini katika maongezi yako.

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Watakaokuzunguka siku ya leo watakuwa na mambo muhimu ya kuongea na wewe si kila jambo linaweza kukufurahisha.

KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23) yoendelea kukupotezea
Achana na wale wenye nia mbaya, weka mkazo kwenye kazi zako na maamuzi yako yabaki kuwa kauli ya mwisho

0 comments:

Post a Comment