SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Mchana
huu ukimuona mtu ana kucha ndefu nzuri, basi ujue hiyo ni ishara ya
kuwa mambo yako sasa yatafunguka na kukunyookea, ile mikwamo ya hapa
na pale itafunguka kwa urahisi.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT
23)
Leo katika matembezi yako ukikutana na mwanamme amevaa mkufu
, hiyo ni dalili ya kupata kila kitu utakachokihitaji bila ya kutumia
muda au nguvu nyingi.Unashauriwa kuwa mtu wa ibada na kutoa
sadaka.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo Mchana
ukikutana Kama Mwanamme huyo akiwa amevaa Mkufu wa Fedha, hiyo ni
dalili ya kutimia kwa ndoto yako ya kupata Mwanamke au Mwanamme mzuri
na kutimia kwa Ndoa yako
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Ukimwona mtoto Mchana huu pua zake ziko safi, basi hiyo ni ishara
ya wewe kupata mtoto mzuri au utapata mpenzi mpya ambaye utakutana
naye bila ya kutegemea. Sherehe utakayohudhuria itakutanisha na wangu
wengi ambao hukutegemea.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES
21)
IkitokeaLeo mtu akaja na akapenga Makamasi nje ya nyumba
yako, basi ujue kuwa ile posa yako imekubaliwa. Unahitajika kuwa
mkweli kwa kila hatua utakayoichukua.
MBUZI - CAPRICORN (DES
22 – JAN 20)
Mchana huu ukipewa habari kwamba kuna mtu
anakusengenya, hiyo ni dalili kwamba utapata yale yote uliyoyategemea
na mtu yoyote hawezi kuwekea pingamizi.tegemea kukutana na mtu mkubwa
Serikalini ambaye atakusaidia.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 –
FEBR 19)
Kama Mchana huu ukiumwa Mgongo au ukikutana na mtu
anaumwa mgongo, hiyo ni isharaya kupata furaha na afya njema.
Vilevile Mkeo au mumeo au mwanao atakufurahisha kwa zawadi
atakayokupa ambayo hukutegemea.
SAMAKI – PISCES (FEB 20-
MACH 20)
Mchana huu akikujia mtu akataka hifadhi ya aina yoyote
kutoka kwako, hiyo ni ishara ya kwamba leo utatukuzwa kwa jambo
utakalolifanya na utapata matatizo katika malengo yako uliyoyapanga
kwa wiki nzima.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Mchana huu
Jumanne, Mdomo wako ukikucheza au ukikutana na mtu ambaye ameumia
mdomo,basi hiyo ni dalili ya kuwa hutafanikiwa katika mambo ya pesa
utakayoyafanya leo.Ili kuepuka hayo jitahidi kumuomba mungu kwa
sala.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Mchana huu
ukimuona Panya katulia mahali wakati si kawaida yake, basi ujue hiyo
ni dalili ya kuwa hauko mbali na mahali ambapo mpenzi wako huwa
anakutania na mpenzi wake mwinngine.
MAPACHA - GEMINI (MAY
21- JUN 21)
Ikitokea leo wakati wowote ukamwona Panya Mweusi
amebanisha mahali kwa muda mrefu bila ya kujitingisha, hiyo ni dalili
ya kukikumbuka kitu ulichokisahau kwa muda mrefu. Mali iliyopotea
siku nyingi itapatikana.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Mchana huu ukimuona mtu ana kucha ndefu, hiyo ni ishara ya
kufanikiwa katika mambo yako ya kibiashara, adui yako atakuogopa na
kukupisha ufanye mambo yako bila ya wasiwasi.
0 comments:
Post a Comment