Wednesday, August 14, 2013

MWAKYEMBE ATEMA CHECHE SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA

 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe ametema cheche juu ya sakata la madawa ya kulevya kupitishwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa JNIA...!

haiwezekani dawa za kulevya kupitishwa kirahisi katika uwanja huo wakati kuna vyombo mbalimbali vya serikali kama Usalama wa Taifa, Polisi, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji na nyingine na wanalipwa mshahara na serikali.

Nilikaa kimya ili kuvipa muda vyombo vya usalama vijiridhishe na kunipa taarifa kutokana na sakata hilo kwani ni aibu kwa uwanja wa ndege wenye jina la Mwalimu Nyerere na nchi kwa ujumla kuchafuka kimataifa kutokana na watu wachache wazembe.

Tatizo hapa siyo mfumo wa mitambo ni uswahili tu ndiyo unaofanyika hapa, leo nitaitisha mkutano na waandishi wa habari kueleza Watanzania wanaofanya hujuma na hatua walizochukuliwa, nataka kuvisafisha viwanja vya ndege ili dawa za kulevya zisipite tena hapo,”

hatua nitakayo chukua itakuwa ni historia na kama wapo watu waliozoea kupitisha dawa za kulevya katika viwanja hivyo labda watafute njia nyingine ya kusafirisha kama ya punda.

0 comments:

Post a Comment