Thursday, August 15, 2013

HIVI NDIVYO ALIVYOFUNGULIWA MASHITAKA SHEIKH PONDA AKIWA KITANDANI WODINI

FFU WAKIWA WAMEJIPANGA KUWEKA ULINZI MKALI WAKATI SHEIKH PONDA ANASOMEWE MASHITAKA JANA AKIWA HOSPITALI.
Jana Jeshi la polisi lilikuwa limepanga kufanya mahojiano na Sheikh Ponda Issa Ponda juu ya kufanya vurugu Zanzibar na Morogoro na askari hao walitarajiwa kutoka Mako makuu ya Polisi ni kwa mujibu wa Juma Nassoro ambae ni wakili wa Sheikh Ponda...!

Lakini siku ya jana badala ya kuhojiwa kama ilivyoelezwa na wakili wake bali alifunguliwa mashitaka akiwa kitandani katika wodi na hali ilikuwa hivi.


Wakati polisi wakimfungulia mashitaka Sheikh Ponda wodini hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kuingia wakiwamo waandishi wa habari na wafanyakazi wa hospitali hiyo.

Taarifa za Sheikh Ponda kufunguliwa mashtaka zilitolewa na wakili wake, Juma Nassoro, ambaye alisema kesi hiyo itakuwa chini ya Hakimu Hellen Riwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu.

Nassoro alisema Sheikh Ponda alisomewa shitaka hilo la kuhamasisha watu kufanya makosa akiwa kitandani Moi ambako anaendelea na matibabu baada ya kudaiwa kujeruhiwa kwa risasi mkoani Morogoro Jumamosi iliyopita.
 

0 comments:

Post a Comment