Tuesday, August 13, 2013

KAULI ZINGINE ZINAUDHI KUMBE POLISI HUWA WANAFANYA MAKUSUDI KUTOTATUA MATATIZO


Leo kama kawaida ya mpitanjia nilipitia gazeti la Nipashe na kukutana na nukuu ya Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova juu ya sakata la mabinti wawili kumwagiwa Tindikali Zanzibar.Kauli ya Kamishna kwangu imeleta maana tofauti kidogo kwani kauli hii inaleta picha kubwa ya uzembe unaofanywa na jeshi la polisi la Tanzania kukabiliana na matatizo mbalimbali.


Tumeona ni hatari sana endapo hatutakomesha haraka mtandao unaojihusisha na uhalifu wa tindikali na ndiyo maana tumeomba tushirikiane  na wananchi ili tukomeshe tatizo hili haraka kabla hatujafika pabaya,
Kumbe Jeshi la Polisi huwa linamukusudi kabsa kwa baadhi ya matatizo kutokuyatatuwa kwa haraka kwa kuwa wao wanaona hayawezi kuwapeleka pabaya?
Aliendelea kutoa maelezo ambayo kwangu sijaona kama ni ya msingi kuliko hizi nukuu akatoa nukuu nyingine tena ambayo bado inaashiria kuwa kuna uzembe mkubwa katika Jeshi la Polisi Nchini katika kutatua matatizo mbalimbali yatokeayo ndani ya nchi.



Hatutaki kuzubaa katika hili, ndiyo maana tumeamua kutoa dau la milioni 100 ili tuwabaini haraka kabla halijatuletea matatizo makubwa kwa sababu ni jambo la kikatili.
Swali langu linakuja hapa hivi kuna majanga mangapi yametokea ndani ya Nchi Polisi ilipiga danadana pasipo kuleta mbwembe zozote zile kwanini hili?
Kumbe sakata la madawa ya kulevya linalowatesa vijana wengi na familia nyingi hapa nchini si la msingi sana kwa kuwa haliwezi kuleta matatizo wala kuwapa matatizo nyinyi? Mbona hamtumii nguvu kubwa juu ya sakata hili wakati iko wazi kabsa kila siku watu hukamatwa na madawa hayo na imani yangu inanituma kuwa watu hao wanaokamatwa huwataja wahusika wanaowatuma katika kazi hiyo,mbona hatuoni mbwembwe zenu katika hilo?






0 comments:

Post a Comment