12:53 AM
Ujumbe huu
ameandaliwa na mtaalamu wa Saikolojia Chris Mauki na ameamuwa
kushare na wewe huu ujumbe ili ujifunze namna ya kuondokana na Stress
zisizo na msingi .
“Haijalishi
unampenda au mnapendana kiasi gani na huyo...! mpenzi wako. Kwa jinsi
mnavyoendelea na mahusiano yenu utagundua kwamba ziko tabia au
tofauti ambazo kamwe huwezi kuzibadili kwake, hatakama unazichukia
kwa kiasi gani.”
Hili litakusumbua
sana mpaka pale utakapoweza kujifunza kuchukuliana na yeye na
kuendana na hizo tofauti tena kwa upendo sio tu kwa uvumilivu. Pamoja
na kukupenda haimaanishi ahadi zote anaweza kuzitimiza kwako, hata
kama amekuahidi kubadilika na kuwa vile utakavyo wewe. Usiliamini
sana hili kwasababu unajiwekea mazingira ya msongo wa mawazo
“stress”.
Na kamwe usifanye
kosa la kufikiri wewe unauwezo au nguvu ya kubadili tabia za mwenzako
ili awe vile utakavyo wewe, Mungu peke yake anaweza hilo, jaribu wewe
uone kama haujafungua milango ya ‘dissapointments’ - Chris Mauki
0 comments:
Post a Comment