Monday, July 29, 2013

KAULI YA MIZENGO PINDA NDIO INAMPELEKA KIKAANGONI SASA..

Kauli aliyoitoa Waziri mkuu Mizengo Pinda Bungeni mwanzoni mwa mwezi huu ya kuwataka Polisi kuwapiga Tu raia ambao wanakiuka taratibu na kutofuata Sheria zitolewazo na Jeshi hilo la Polisi wawapokazini katika kuzuia vitendo vya Fujo....!


Uchokozi au kuzuia vitendo vyovyote vinavyoashiria kuvunjika kwa amani,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinatarajia kumfikisha mahakamani Waziri Mkuu kikimtaka atengue kauli hiyo aliyoisema mbele ya Bunge la Jamhiri ya Muungano wa Tanzania.
Mwezi uliopita Pinda katika mkutano wa Bunge la bajeti mjini Dodoma alitoa kauli ya kulitaka jeshi la Polisi nchini kuwapiga raia wanaokaidi amri halali ya jeshi hilo wakati aikijibu maswali ya Papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.


Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia, alisema taratibu zote za kisheria za kumfikisha Pinda mahakamani zimekamilika na siku yoyote wiki hii watafungua kesi.

Kiukweli kauli ya Pinda, imevunja katiba ibara ya 13 na kwamba lazima sheria ichukue mkondo wake kwa mkumfikisha mbele ya mahakama.

Alifafanua kuwa ibara ya 100 inayompa kinga mbunge anapotoa jambo lolote bungeni inamweka kando Pinda, kwa kuwa yeye hakuzungumza bungeni kama mbunge bali alikuwa anatoa msimamo wa serikali yake.


 Alisema kauli ya Pinda ilikuwa kali na mbaya na kwamba, walimtaka Pinda aifute siku chache baada ya kuitoa, lakini mpaka sasa amekaidi na hivyo wameamua kuchukua hatua ya kumfikisha mahakamani ili haki iweze kutendeka.



0 comments:

Post a Comment