Nianze kwa kutoa pongezi kwa Ben Paul na
Producer wake Lucci kwa kuweza kufanya kazi nzuri ambayo ni inspiration Song
kwa vijana wa Kitanzania,Ben paul katika ngoma hiyo ameonesha uwezo wake wa
Hali ya juu sana pamoja nae Lucci katika kuikamilisha ngoma hiyo.
Lakini baada ya Ngoma hiyo kufanikiwa na
kupokelewa vizuri na jamii kuna ngoma kama hiyo ya Inspiration pia yenye
midundo ya ngoma ya Jikubali ya Ben Paul,yenye Idea ya inayoelekeana nay a
Jikubali hata Stlye ya Kuimba ambayo ni ya Msanii The Script
akiwa amempa Shavu will.i.am na ngoma
inakwenda kwa jina la Hall Of Fame .
Sina tatizo na Ben Paul wala Lucci ila
tatizo langu lipo katika kitu kimoja kinaitwa Attribution si vibaya kucopy au
kurudia ngoma yoyote ile maana hata kwa wenzetu wanafanya hivyo ila unapaswa
kusema kuwa hicho kitu ni cha mtu na wewe umekirudia tuu ili hata kama unapata
credit kwa kazi hiyo tunakuwa tunajua chanzo chake kipi lakini ndugu zangu hawa
wamefanya kazi kama yao na kupiga kimya kama wao ndio wameifanya kazi hiyo
mwanzo mwisho.
Kwa hili Ben paul na Lucci hamjatenda
haki tunaitaji nyinyi muwe mfano wa kuigwa kwa kuwa mnafahamu mambo ya Haki
miliki jinsi yanavyokwenda,mna elimu ambayo inaweza kuwasaidia kujuwa hicho
mlichofanya,sasa kama nyinyi mnafanya hivyo kina Nanii wafanye nini sas?
Nisionekane kama nimewaundia hoja nanyi
mshuhudie wenyewe kazi waliyocopy japo kiuwezo Msanii Ben Paul na Lucci wapo
vizuri na hakuna anaebisha katika hilo. BOFYA LINK HIII NA UTAJIONEA MWENYEWE.http://www.youtube.com/watch?v=jukv9Q1eR2g
0 comments:
Post a Comment