Wednesday, May 1, 2013

NYOTA YAKO LEO JUMATANO: 1/5/2013



NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Siku ya leo usipokea au kukubali kitu chochote ambacho cha kugushi au cha uongo unapata bala. Inaonyesha kwamba unawaamini sana watu katika biashara, mapenzi au kazi , unatakiwa uangalie upya uhusiano wako na watu hao.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Ikikutokea Leo ukasimamishwa ghafla na Mtoto, hiyo ni dalili kwamba mpenzi wako uliemuacha atajaribu kuvuruga heshima yako kwa watu., hata hivyo ukisimamishwa ghafla na Mwanamke, au Maskini au Rafiki unayemfahamu tegemea kupata faida ya Pesa au Utawala.
.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Siku ya leo ukishutumiwa na kama ikiwa hujui lolote kuhusu shutuma zenyewe, hiyo ni ishara ya kwamba ujichunge unaweza kutumiwa na watu wabaya katika kutekeleza malengo mabaya.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Ikitokea leo Kama unashutumiwa na shutuma zenyewe zimewekwa wazi au bayana na wewe umeweza kujitetea na kuthibitisha kwamba huna hatia, hiyo ni ishara kwamba utapata matatizo ambayo utaweza kupambana nayo na kuyashinda.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Siku ya leo ukimpata Mshirika mpya au kama ukikutana na mshirika wako wa zamani, hiyo ni ishara kwamba utazigundua fedha zako au kitu cha thamani ambacho ulifikiria kwamba umekipoteza na kuongezeka kwa shughujli zako za kijamii.


MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Wiki hii ukipata habari ya mtu unayemjua kuachiwa Mahakamani hiyo itakuwa ni ishara ya kupata Upinzani kutoka sehemu nyingi, iwe Kazini , Nyumbani, katika Mashindano na Kadhalika, hata hivyo unachotakiwa kufanya ni kujituliza na upinzani huo wote utapotea.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Ikiwa wewe mwenye nyota hii una mapenzi ya kweli kwa mtu au kitu kwa mfano Mumeo, Mkeo, Watoto, Dini, yako gari na kadhalika, hiyo ni dalili ya kupata Amani na mafanikio,

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Ikikutokea leo Ukaona una mapenzi katika jambo au kitu ambacho wewe unakiona kama hakifai kuoneshwa mapenzi kama hayo, hiyo ni dalili kwamba utapata mfadhaiko mdogo katika mambo yako.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Siku ya leo ukikuta chombo kinaelea kwenye maji, hiyo ni ishara ya kushindwa kuyatatua matatizo yako uliyokuwa nayo, au unaona taabu kuyakabili matatizo hayo.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Leo kuna dalili kupata wakati mgumu mbele yako, Pia kuna uwezekano wa kutokea maziko ya jirani au mtu unayemfahamu kati ya sasa na wiki mbili zijazo.ukipata habari na mtu aliye jela basi utasafiri.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Mwezi huu kuna dalili ya kupumzishwa au kuachishwa kazi au kupata matatizo ya kikazi.hasa ukiona taa Chemli inawaka mchana ikiwa umeiwasha wewe na ikazimika ghafla basi ujue kuna ugomvi

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Mpenzi mpya ambayo atakuwa anakupenda na utafunga naye ndoa. Utakutana nae kati ya Siku ya leo na kumamosi ijayo. Jaribu kuwa karibu na adui zako watakusaidia katika mipango yako ya kimaisha

0 comments:

Post a Comment