Wednesday, May 22, 2013

NYOTA YAKO LEO ALKHAMISI; 23/5/2013



MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21) 
Leo ukikutana na mtu akakuambia ana njaa na anahitaji chakula, hiyo ni dalili kufanikiwa katika mambo yako, pia kazi zako zitasifiwa na wakubwa wako na utajikuta ukipewa zawadi bila ya kutegemea. 

KAA – CANCER JUN 22 – JUL 23
Leo ukipata salamu kutoka kwa rafiki aliye mbali au akija ghafla au ukikutana naye njiani, hiyo ni dalili kuwa mambo yako yatakuwa na mikwamo ya hapa na pale hasa inayohusiana na mapenzi, unashauliwa kuwa mtulivu na kupanga mambo yako kwa uangalifu sana.

SIMBA – LEO JUL 24 – AUG 23
Leo ukikutana na ndugu yako ghafla, hiyo ni dalili kuwa utapata habari mbaya bila ya kutegemea pia mambo yako uliyopanga yatakwama. Pendelea kufanya ibada na kutoa sadaka

MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Leo ukimuona mtu anapelekwa mahakamani, hiyo ni dalili kwamba mambo yako yatakuwa mazuri na hasa kama una kesi basi ujue utashinda kesi hiyo, Jaribu kusikiliza maoni ya watu.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Leo ikikutokea ukaumia bila ya sababu, hiyo ni dalili kwamba mambo yako yatakuwa siyo mazuri hata kidogo, unatakiwa kuwa mwanagalifu kwa kila jambo unalotaka kulifanya, makosa kidogo tu yanaweza kukusababishia hasara ya mali au kupata ajali.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo ukikutokea ukamwagikiwa na rangi au ukimuona mtu amemwagikiwa na rangi, hiyo ni dalili ya kwamba kuna watu wanakuzunguka katika mipango yako, unashauliwa kuwa makini na watu unaoshughulika nao kwani wengine si wema kwako.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV23 - DES 21)
Leo katika matembezi yako ikitokea ukakutana na Mwanamke kwenye kona amebeba maji, hiyo ni dalili kwamba mambo yako yatafanikiwa na utajikuta unapata pesa hata kwa kazi ambayo hukutegemea kupata pesa.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo ukipata Mwaliko wa shughuli ya kidini , iwe Kanisani au Msikitini , hiyo ni dalili kwamba mipango yako iliyosimama kwa muda mlefu sasa itafunguka na kufanikiwa.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Leo katika matembezi yako ukisikia mlio wa maturumbeta, Hiyo ni dalili ya kwamba mambo yako yatakuwa mepesi na migogoro iliyoibuka kati yako na mpenzi wako au kazini kwako itamalizika.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo ukikutana na mtu anapiga kinanda, hiyo ni dalili kwamba kuna mtu ana hamu ya kufanya urafiki na wewe, unashauriwa kushirikiana naye kwani kuna manufaa makubwa utayapata kwake.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo ukimuona na mtu anajificha, hiyo ni dalili kuwa mambo yako mengi yataharibika au utajikuta ukitafuta vitu kwa muda mrefu bila ya kuviona, lakini baada ya kukata tamaa unakuja kuviona mahali ambapo huamini.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Mchana huu ikitokea ukamwona Farasi , hiyo ni dalili nzuri kwako kibiashara au kikazi.Tegemea kupata rafiki mpya au kumpata mpenzi atakayekuwa mshauri wako mkuu.

0 comments:

Post a Comment