Mbunge wa Kigoma Kasikazini Mh Zitto Kabwe ameyashukia makampuni
ya Simu kuwa wanapaswa kulipa kodi ya mapato bila kuangalia aina ya uwekezaji
walioufanya nchini.
Zitto ameyasema hayo kufuatia Kauli ya serikali waliuoitoa
kuwa makampuni ya simu Nchini yanalipa kodi nyingi,kufuatia kauri hiyo Zitto
alihoji kodi gani inayolipwa na makampuni hayo? VAT! Nani kasema VAT inalipwa
na kampuni?Hii Ni kodi ya walaji
kama ilivyo ushuru wa bidhaa (excise duty).
“ Serikali inasema kampuni za simu hazilipi kodi ya mapato
Kwa kuwa zimewekeza sana, Tshs 2.5 trilion! Nani kakagua huo uwekezaji? Eti Kwa
miaka 5 kodi ya makampuni iliyolipwa Ni Tshs 64 bilioni, ambayo ni wastani wa Tshs 12 bilioni Kwa mwaka.”
Aliendelea kukaliliwa akisema kuwa kwa Nchi kama Rwanda yenye
idadi ndogo ya Wananchi ambapo ukilinganisha na Tanzania ni sawa na wateja ya
Kampuni moja ya simu lakini wao Nchi yao ililipwa kodi ya juu zaidi kuliko
Tanzania hivyo aliitaka serikali ya Tanzania kuacha Utani na Blah blah katika
vitu vya msingi na vyenye masirahi kwa Taifa letu.
“Rwanda yenye idadi ya
watu sawa na wateja wa Vodacom peke yake mwaka 2010 walikusanya corporate tax
$14m, Tanzania ilikusanya $1.4m tu. Serikali iache blah blah, ikusanye kodi.
TCRA ipewe Nguvu ya kukagua uwekezaji wa makampuni kama ilivyo TMAA kwenye
madini. Inatosha sasa”






0 comments:
Post a Comment