Na Kitalima Gerald
MTAYARISHAJI
wa muziki wa Bongo flavor na mmiliki wa Studio ya BURN Records Sheddy Clever
Amefunguka na kusema kuwa Bila mama yake mzazi(Rebeca)Angekua ameshakata tamaa
na kuachana na masuala ya kutayarisha muziki.
Sheddy Clever amesema hayo kufuatia support kubwa
anayoipata kutoka kwa mama yake Mzazi kimawazo na ushauri pindi anapopata
changamoto katika kazi yake ya utayarishaji wa muziki na maisha Kiujumla.
“Mama yangu ndio kilakitu na mafanikio niliyopata
kimuziki basi mama anamchango mkubwa sana kwani kunakipindi nilipigiwa simu za
vitisho mpaka kufikia hatua ya kutaka kuachana na Muziki lakini Bimkubwa alinishauri
kusimamia katika kitu nachokiamini nitafanikiwa tu.
Sheddy Clever alietengeneza HITS kama
Zilipendwa(Matonya),Mary me(Mavoko) Nivute Kwako (Dyana) Amekua (Pasha$Tunda Man)
Ameweka wazi Alikua na Mpango wa kufanya kazi na Diamond Platinum na Mpaka sasa
Anaona hizo ndoto Zipo njiani Kutimia kwani teyari amekwisha tengeneza Beat na
Diamond Platinum.
AKizungumzia Ushirikiano kati yake na
Watayarishaji Wengine wa Muziki Nchini Tanzania Amesema kuna baadhi yao
wanaushirikiano mzuri mno lakini wengine ni Tatizo
SHEDDY CLEVER KWA POZI |
“Kiukweli kabisa kuna producers kama MAN WALTER
Ana roho nzuri sana yeye kanipa support sana kimawazo hata kunifunza vitu
vingine, kiukweli Big up kwake lakini kuna baadhi ya producers hawafanikiwi
kutokana na Roho mbaya zao.
0 comments:
Post a Comment