Wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Nairobi wamelalamikia ongezeko la kunguni katika
vyumba vya kulala chuoni. Wanasema kunguni wameongezeka mno hasa
katika vyumba vya kulala vilivyojengwa kwa mbao, almaarufu 'Prefabs,’
vinavyotumiwa na wanafunzi wapya na wa mwaka wa pili.
Wanasema
kunguni wameongezeka mno hasa katika vyumba vya kulala vilivyojengwa
kwa mbao, almaarufu 'Prefabs,’ vinavyotumiwa na wanafunzi wapya na
wa mwaka wa pili.
Kulingana
na wanafunzi hao, vyumba hivyo vimevamiwa na kunguni kutokana na
idadi kubwa ya wanafunzi na kupelekea hali mbaya ya usafi.
“Kunguni
wamekuwa wengi sana msimu huu,” alisema Bw Joseph Maina kiongozi wa
wanafunzi chuoni.
Wanafunzi
walishtumu usimamizi wa chuo hicho kwa kuzembea katika kudumisha
usafi wa wanafunzi wanaozidi kuongezeka kila mwaka.
Chumba
kimoja hutumiwa na wanafunzi watano au hata zaidi. Kuna msongamano
mkubwa wa wanafunzi unaofanya usafi kudorora na maisha katika vyumba
hivyo kuwa magumu,” akasema Dominic Thuva mwanafunzi wa mwaka wa
pili.
Wanafunzi
wapya waliokuwa wakisajiliwa Jumatatu walionekana wakikagua godoro
hizo pamoja na wazazi wao kabla ya kuanza kuzitumia.
Baadhi
ya wanafunzi pia walihusisha kunguni hao na kutobadilishwa kwa godoro
zilizotumiwa kwa muda mrefu.







0 comments:
Post a Comment