9:47 PM

NG’OMBE – TAURUS (APR 21 –
MAY 20)
Kuna dalili kwamba mpenzi wako atakughasi kwa maneno
maneno kila wakati kuhusiana na uhusiano wako nje ya ndoa. hata kama
wewe utakanusha lakini yeye bado atashikilia msimamo wake kwani
amepewa habari za uhakika. Jaribu kuwa mpole ili balaa liishe..
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Mambo yako uliyoyapanga
ili kupata pesa wiki hii yatasimama au kuwekewa vikwazo vya hapa na
pale. Na watakaofanya hivyo ni watu wako unaowaamini. Jaribu kuachana
na mipangi hiyo mpaka baadae.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Kuna mpenzi wako alie mbali na wewe unamkufikiria sana. Elewa
kuwa mpenzi huyo yupo njiani anakuja kukutembelea na kukuletea
msaada.Jaribu kuweka mambo yako sawa ili akija akute kila kitu
kizuri. Utapata faida kubwa kwake.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG
22)
Ile mikosi inayokuandama nyumbani na kazini itaendelea tena
wiki hii. Ili Kuondoa hali hiyo pata msaada kutoka kwa
watalaamuwakusafishie nyota yako, vinginevyo mambo yako yatakuwa
mabaya zaidi.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Usipokuwa
muangalifu katika siku mbili hizi kuna dalili ya kumpoteza mpenzi
wako wa muda mrefu, Inaonekana pia kuna dalili ya kupoteza kitu chako
cha thamani sana, chunga sana hali ya kusahausahau.Weka vitu vyako
vizuri.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Elewa kuwa kuna
mpinzani wako wa karibu asiyependa maendeleo yako. Anajaribu kila
njia kukutafutia mabalaa.Unashauriwa ili kuepukana na hayo ni vyema
ukahama sehemu uliyopo hivi sasa.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV
22)
Siku ya leo katika matembezi yako ukikutana na mtu amebeba
Samaki, hiyo ni dalili kuwa mambo yako yatafunguka, Lakini unatakiwa
kuwa makini sana na watu watakaokujia na kutaka msaada kwako, kila
samaki mmoja utakayemuona ni Bahati moja nzuri.
MSHALE -
SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Siku ya leo jitahidi sana
kujibidiisha na kufuatilia mipango yako. Maombo yako yote uliyopanga
yako tayari isipokuwa kuna mtu anayashilikia. Jaribu kuzungumza nae
hata kama ikiwa ni kutoa kitu kidogo ili yawe sawa, wewe toa. Faida
ni kubwa kuliko hasara.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Usiwe muoga kutoa msadaa kwa matatizo yanayowapata wenzio hasa
kama mkiwa mmeongozana pamoja. Jaribu kurekebisha hiyo tabia yako ya
ubahili mara moja vingenevyo itakuleta balaa.uktakapotoa ndio
utakavyopata.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Leo
kuwa muangalifu sana unaweza kuletewa biashara ambayo itakuletea
balaa kimaisha. Biashara yoyote kwa leo haifai. Kuhusu kazini kuna
mtu anakuchimba anataka ufutwe kazi jaribu kufanya mambo yako kwa
makini hasa kazini.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Ile
biashara unayotaka kuifanya na uliipanga wiki hii itakuletea faida
kubwa ambayo itakusaidia katika mipango yako ya baadae. Yale makosa
yako na madhambi uliyomfanyia rafiki yako au utasamehewa Jaribu kuwa
muangalifu.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo Kuna dalili
za kuletewa zawadi kutoka kwa rafiki yako. Zawadi hizo zitakufariji
sana. Ile migogoro yako katika mapenzi itakwisha hivi karibuni na
kama ulikuwa unaugua au unauguza mgonjwa basi utapona na mgonjwa wako
atapata nafuu haraka.
Imeandaliwa na Mtabiri Maalim Hassan
0 comments:
Post a Comment