Msanii
matonya kutoka pande za Tanga anaepiga mzigo katika tasnia yamuziki
wa Bongo Fleva ametosa kufanya show ya miaka 13 ya Lady jaydeeshow
ambayo itarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa ya Tarehe 31 May.
Kwa
mujibu wa Captain amesema kuwa Matonya alichukua Advance na
kukubaliana kushiriki siku ya show lakini baada ya watanzania kupewa
taarifa kuwa matonya angeshiriki show hiyo alitoa taarifa ya
kutoshiriki show hiyo kwa kutoa sababu ya kuwa hajafanya maandalizi
ya kutosha kufanya show kwa Band .
Baada
ya kutoa taarifa ya kutoshiriki aliombwa kuludisha kiasi cha pesa
alizochukuwa kama Advance lakini Motonya hakuweza kufanya hivyo
“Lakini
tetesi zinasema kuwa Matonya alipigiwa simu na wazee wa fitna mara tu
waliposkia kluwa atashiriki onyesho la miaka 13 ya JayDee,
wakamwambia aachane na hiyo show na kuwa watampa hela ambayo
angelipwa kwenye show hiyo.
Na
pia wangemuandalia show yake mwenyewe kubwa zaidi ya hiyo miaka 13 ya
JayDee
Hizo
ni fununu, ambazo hazina uhakika.
Lakini
tukirudi upande wa Matonya ambae alishapokea mpaka malipo ya awali na
kukubali kufanya show baadae akachomoa ni kama ifuatavyo.”
MAZUNGUMZO
KATI YA CAPTAIN NA MATONYA YALIKUWA HIVI
CAPTAIN:
Ni Ijumaa tar 31 May 2013 kaka mwezi ujao. Tutakuwa na Linah, Jay,
Barnaba, Matonya, TID, hamza Kalala
MATONYA:
Kaka kumradh sana kuimba na band kwasasa sitoweza manake mtaitaji
mandalizi makubwa ili nifanye kazi vzr_ningeomba nitizamwe ktk kazi
ingine bro kumradh sana
CAPTAIN:
Du! Nshatangaza ilikuwa kaka lakini sawa. Je ntapata ile hela kka
nilipe wengine ndg yangu
MATONYA:
Aisee hata nimekosa raha kukujuza iliswala br_kesho satano mtampa
yule rafkiangu anaitwa pizon_walikuja kuleta ile pesa yagari kwaio
wataileta apo apo oficen
CAPTAIN:
Sawa kaka usijali, Nitashukuru akiileta ili huku nisipate lawama
MATONYA:
ok bro
Mara
kimyaaaaaaa....... baada ya siku mbili tatu maongezi yakaendelea
CAPTAIN:
Naam kaka mzigo haujaletwa. Tafadhali ileteni tu hiyo hela ya watu
kaka mi napewa lawama isitoshe we ni ndugu yangu usikubali hela ndogo
iharibu.
MATONYA:
Gadna aiwezi kuwa ivyo_kuna mapungufu kidgo nayaweka sawa uipate
kumradh sana brother
CAPTAIN:
Asante
Siku
ikapita tena
MATONYA:
Kaka kdg kunamisteki nimecheza,, lakini wiki hii haitapita mtakuona
bro nimekwama kaka lakini ntajua cha haraka
CAPTAIN:
Sijaelewa kaka ni laki **** tu kunirudishia nduguyo nilipe wasanii
wengine kwani kuna tatizo au
MATONYA:
Bro naskia haya - skutaka hata kuku2mia msg mlitaka ni2we namzigo 2
ila kunambio kdg zimekwamisha nikaona bora kukujuza kuliko kukaa
kimya bro tatizo haliwezi
CAPTAIN:
Sawa we ni ndugu yangu, basi nisaidie tu irudi hiyo advance
niliyokupa ili uniepushe na lawama huku kaka. Au niende kwa bimkubwa
Tanga nikalalamike? Ha haaaa haaa
CAPTAIN:
Fanya hivyo mdogo wangu nilitaka uwepo ktk show kwa upendo tu lakini
haijawa, basi nisaidie tu kurudisha hiyo advance maana nadaiwa na
wasanii wengine niwape. Au sio?
MATONYA:
Kaka nibendi ndio haya yangu kwasasa nastaki kuharibu kaziyako bora
niwe mkweli.. Naswala lako halitoki kichwani bro
CAPTAIN:
Sawa jamaa yangu, basi nisaidie ile advance irudi ili niweke mambo
sawa huku, mimi sina mdhamini mpaka leo aliyetoa hela, najitegemea tu
mfukoni, naomba nirudishie nilipe wengine..Au namoro matonya we ni
ndugu yangu?
MATONYA:
Sawa brother mtalisimamia soon nikuweke sawa sawa brother - akuna
litakalo shindikana kaka amini 2
CAPTAIN:
Utarudisha lini nipe uhakika kaka, niko na shida
Adavance
ilitoka tangu mwishoni mwa mwezi April
Mazungumzo
ndio kama hayo mmeyasoma
Mpaka
blog inaingia mitamboni leo, advance haijarudishwa na hakuna jibu la
kueleweka.
Wazee
wa fitna kama zile tetesi ni kweli kuwa mmemzuia Matonya asifany hii
show ya miaka 13 ya JayDee, na hela ameshaitumia! Kwanini msimsaidie
kuirejesha mambo yaishe??







0 comments:
Post a Comment