Na
Kitalima Gerald
KATIBU
wa JKT Ruvu David Ngaga amekili kuwa
katika mzunguko wa kwanza wa Ligi timu ya JKT Ruvu ilifanya makosa katika mechi
mbali mbali ilizocheza .
Akizungumza
na Champion jumatatu David Ngaga amesema
wamebaini makosa mbalimbali katika mechi walizopoteza msimu wa kwanza wa
ligi na kuamua kufanya usajili katika dirisha dogo na kuongeza wachezaji watano
katika kikosi cha JKT Ruvu .
“Tulifanya
makosa mwanzo hatukua na viungo washambuliaji wakutosha lakini tumetambua
makosa na wachezaji wametambua makosa
yao hali hii ndio imepelekea kuwaongeza washambuliaji wengine watano katika kikosi cha JKT Ruvu
akiwemo Mussa Mgosi na Zahoro Pazi
“Mbali
na kina mgosi kuna Kiungo mshambuliaji wa kushoto Immanuel Pius,Nashoni Naftal
na Beki Kisimba Rwambano ambao teyari wamekwisha anza mazoezi chini ya Kocha Charles Kilinda
Katibu
David amesema kuwa anatambua JKT Ruvu
inakibarua kikubwa kutokana na makosa yaliyotendeka lakini anaimani kubwa sana
kuwa kwa kikosi walichonacho sasa wanaweza kupata zaidi ya points saba.
“kwa
sasa JKT Ruvu tumejipanga kupata points saba zaidi na kwa kikosi chetu cha sasa
naamini hakuna litakaloshindikana maana
wachezaji wanajiandaa vyakutosha kwa msimu wa pili wa Ligi huku wakijua ni nini wakifanyacho.
JKT
Ruvu walifungwa magori 3-0 na Azam FC
walipocheza mechi ya kirafiki Katika
uwanja wa Chamazi Kabla Azam FC hawajaelekea Zanzibar kwa mashindano ya
Mapinduzi.







0 comments:
Post a Comment