Na
Kitalima Gerald
MWENYEKITI
kamati ya Uchaguzi TFF lyatto amesema kuwa mchakato wa kuwatafuta viongozi wa
Tanzania Premier League Board umeanza rasmi na uchaguzi utafanyika tarehe
Ishirini na mbili mwezi wa pili jijini Dar es salaam.
Akizungumzia
nafasi za kugombewa ni pamoja na
Mwenyekiti wa TPL Board,Makamu Mwenyekiti wa TPL Board,pamoja na Wajumbe
wawakilishi wa Klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL
Board ambazo ni nafasi mbili.
“Fomu
za maombi zitaanza kutolewa tarehe kumi na nne mwezi huu kutoka kwa Katibu wa
Kamati ya uchaguzi ya TFF(Katibu Mkuu)
na mwisho wa kuludisha fomu ni tarehe kumi na nane ya mwezi wa kwanza,fomu
ya mwenyekiti na makamu Mwenyekiti itaghalimu
Shillingi Laki Mbili wakati fomu ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TPL ni
Shillingi Laki MOja.







0 comments:
Post a Comment