Friday, January 11, 2013

Lyato, katiba TFF haizuii Kugombea



Na Kitalima Gerald 

MWENYEKITI  kamati ya Uchaguzi TFF Deogratias lyato amedai kua Katiba ya TFF haimzuii Kiongozi yeyote yule aliyepo Madarakani kugombea nafasi yoyote ile katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.
Lyato amesema kuwa  hakuna kipengele chochote kile katika katiba ya TFF kinachotoa pingamizi kwa kiongozi aliyopo madarakani zaidi ya mara mbili kugombea tena nafasi yoyote ile katika shirikisho hilo.

“hakuna kipengele chochote kile katika katiba ya TFF kinachoweka pingamizi kwa kiongozi yeyote aliyopo madarakani kwa mara kadhaa kugombea nafasi kwa mara nyingine tena ila kunakipengele kinachozuia mtu akiwa na umri chini ya miaka ishirini na nne (24)

“kwa upande wa mgombea wa Uraisi TFF ikiwa mgombea amezidi Umri wa miaka sabini na tano (75) katiba hamruhusu kugombea, mbali na kigezo cha Umri hakuna kipengele kingine kinacho mzuia mtu kugombea nafasi yeyote ile katika shirikisho la mpira wa miguu Tanzania”

Lyato imebainisha kuwa kama kuna kiongozi yeyote yule aliopo madarakani kwa sasa au kaongoza shirikisho hilo kwa mara kadhaa ikiwa hata gombea katika nafsi za uongozi katika uchaguzi utakaofanyika 24 mwezi wa pili mwaka huu utakua ni utashi wake mwenyewe kutogombea kama kigezo cha umri hakijawa pingamizi kwake.

“kiongozi yeyote yule aliyopo madarakani kwa sasa katika Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania kama hatogombea basi ni utashi wake mwenyewe kutogombea “

0 comments:

Post a Comment