Mwandishi: GERALD KITALIMA
TELEPHONE NUMBER:0717-199561
Badra na
basil ni wanafunzi wa chuo kikuu cha st.agustine mwanza,wakiwa chuoni hapo
basil hufahamika sana kwa walimu na wanafunzi wenzake sababu ya fani yake ya kuimba
yaani ni msanii mwimbaji,hali hii ilimpelekea kupendwa na vijana wengi wa
jinsia zote hapo chuoni na baadhi ya walimu walio tambua kazi na mchango wa
basil katika kuwakusanya raia na kuwapunguzia stress za maisha pale awapo
stejini akiimba nyimbo zake hata kufanya copy ya nyimbo nyingine za wasanii
wengine.
Badra
hakuwahi hisi wala kuzania kama siku moja anaweza kuwa kalibu na basil hata kwa
kupiga stori tuu,hii inaonesha jinsi gani basil alikua mtu wa dhamani kwake
yaani kifupi badra alijihisi kuwa yeye asingekua na hadhi hata ya kuongea na
basil.laahasha usilolitambua ni sawa na usiku wa giza,badra alikua na utamaduni
wa kwenda club na katika kumbi mbalimbali za starehe ifikapo week end,hivyo
basi siku ya jumamosi kulikua na tamasha basil aliudhulia tamasha hilo kama
mwanafunzi na wala si msanii akiwa na jamaa zake wakipeana support kushangweka
kiujanja zaidi.
Badra pia
alihusika kwa namna moja katika tamasha hilo hivyo alitokelezea kwa lengo la
kula bata na kupunguza stress za masomo badra hakuwa alone nae alifuatana na
mashostito wa town wanaotokea pande za college mpaka hapo najua ushawajua kuwa
ni masister duu ndio nawazungumzia,lakini cha ajabu makundi yote mawili
yalifika muda sawa na wakiwa wamechelewa tulipo waona kwa mbali tulijua
wametokea kiwanja kingine hapa wamefika kumaliza shughuli tuu,lakini kadili
walipo sogea ndipo tukabaini kuwa hakukua na uhusiano wowote ule kati ya kundi
la masharobaro wa college na masister duu wetu wa chuo.
Kwa ule muda
waliofika viti na meza zote zilikua zimesheeni raia wa kutosha,wakiwa katika
hali ya kutahamaki mhudumu alikuja na meza moja na kuwawekea pale na kuwaambia
kuwa itawabidi wa share meza kwani ndiyo ilikua meza ya mwisho,haikua ngumu
kwao sababu kusudio lao ni kula bata ndefu,waliletewa viti na kuhudumia
vinywaji,baada ya vyombo kuanza panda kichwani ndipo ulikua wakati wa
kutambulishana na kufahamiana vizuli,badra alijikuta akipiga stori na mtu ambae
kamwe hakuwaza kama ingekuja tokea hata wakaongea kwani yeye alimuona kama
mungu mtu kwa jinsi basil alivyokuwa akiji brand mwenyewe.
Hii ilikua ni
nafsi ya kila mmoja kufahamiana na wenzake na kubadilishana mawazo,hapo ndipo
urafiki ulipo anza kati ya basil na badra wakiwa chuoni na hii ndiyo ilikua
tiketi ya mahusiano kati ya wawili hawa,baada ya maongezi ya muda mrefu
walibadilishana number za simu,lakini nafsi na roho ya badra ilitawaliwa na
furaha ndani yake kama ameokota fuko la mshahara,jamani nadhani tunajua pindi
tupatapo nafasi ya kuwa kalibu na mtu ulie hisi huwezi pata nafasi ya kuwa nae
kalibu kutokana na umalufu wake bhanaaa.
Mawasiliano
ya kalibu yalijengeka kati ya wawili hao ndani ya siku tano tuu,weekend
iliofuata basil alimualika badra chakula cha jioni,siku ilipowadia basil
alimkumbusha badra na kukubalina saa kumi na mbili na nusu wakutane sehemu
husika,basil aliendelea na majukumu yake ya kila siku kwani alikwenda studio
kwanza kuingiza vocal tetemesha records chini ya producer wake kidbway,lakini
ratba ya kuingiza vocal ilihalibika kwani akiwa studio walitokea wanamuziki
kutokea dsm wanaume family hivyo walitaka kufanya truck na kuondoka siku
inayofuata na kuicha ikiendelea andaliwa.
Basil aliambiwa na kidbway asubili kidogo
asiondoke,alisubili kwa muda mrefu bila mafanikio hivyo alilazimika kumtoloka
producer wake ili akatimize malengo yake ya kuonana na badra,lakini hat hivyo
kwa muda aliotoka alihisi angechelewa,hakuwa na budi kukodo boda boda ili
aepuke foleni njiani,akiwa njiani basil alipata ajali ya pikipiki aliumia na
kupelekwa hospitali ,akiwa njiani na katika maumivu makali aliota simu yake na
kuwaomba watu wampe taalifa badra kuwa amepata ajali na anaelekea hospitali.
Badra
alishtushwa na taalifa ile hivyo alichanganyikiwa na kuuliza mambo mara nne
nne,ahhha kwa hiyo hajaumia sanaa,vipi yupo hospitali gani,jamani saa ngapi
kapata ajali mbona mimi nimeongea nae kwenye simu,pindi yanaulizwa maswali haya
badra alikua akionesha alikua anabubujikwa na machozi kwani promise imegeuka
maumivu moyoni mwake kwa kupata taalifa isiyo nzuli kwa yule ampendae kwa
dhati.badra alichukua jukumu kuhakikisha anafika hospitali usiku ule,akiwa
katika hali ya sintofahamu alifanikiwa kufika hospitali kumuona basil akiwa poa
kiasi baada ya kupewa matibabu……………itaendelea






0 comments:
Post a Comment