Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha tumaini university dar es salaam TUSODARCO,Naifananisha na toroli bovu lisilo tembea na lililo shindwa kubeba mzigo na kuelemewa na mzigo mzito.
Hii
inajidhirisha wazi kutokana na uteuzi
mbovu wa viongozi katika serikali hiyo,kuanzia ngazi ya chini ya uongozi mpaka ngazi ya juu uongozi katika
wizara zake,kwani uteuzi huo ndio umekua chanzo cha mambo mengi kushindwa kufanyika, hata kama hufanyika lakini haku kidhi haja na mahitaji ya wanafunzi,hii si
mara ya kwanza kwa kiongozi mkuu wa serikali hiyo kufanya uteuzi mpya katika
baadhi ya wizara kwani awamu ya kwanza alimtoa madarakani waziri wa mikopo na
kumpa wadhifa huo mtu mwingine,kama
kweli mh:Rais uliamua kuchukua jukumu zito kama hilo hukutambua toka awali
kwamba waziri huyo hakuwa na vigezo vya kuwa waziri wa bodi ya mikopo?
Chanzo
changu cha habari kinanipasha kuwa,Rais wa serikali ya wanafunzi amekua na
silka,hulka ya kuteua viongozi kwa kuzingatia”USWAHIBA”,kwa hali hii mkuu wangu hutaweza kusukuma kurudumu la
maendeleo kwa wanafunzi wa tumaini university kama inavyofahamika huwezi kuwa
mtendaji mzuri wa shughuli za kiserikali ikiwa boss wako ni jamaa yako,utafanya
uzembe,makosa lakini mwisho wa siku hawezi kukudhuru kwa jambo lolote lile,nakukumbusha
tu wazungu husema,
THE BEST FRIENDS ALWAYS IS THE ONE
WHO LET YOU DOWN,hili
kichwani likuingie mh:Rais.
Nikukumbushe
tuu mh: wanafunzi walikua na imani kubwa
sana na uongozi wako kabla hujaingia madarakani wakijua kuwa utakua mtetezi
wao kwa matatizo yao,lakini mambo yamebadilika kwao kwa sasa,wanafunzi walianza
kuwa na mashaka na serikali yao pindi tuu ulipotangaza baraza lako la mawaziri
na serikali yako kiujumla ,imani ya wanachama wako umeichoma na kuiteketeza kwa
maamuzi yako mwenyewe na washauri wako kwa kuwaacha
watu dhabiti na wachapa kazi mahili na kuamua kukumbatia gunia lenye
misumali linalo kupa maumivu makali.
Nini
maana ya serikali yako ikiwa siri bayana
zinawekwa wazi,na mambo yasiyo ya siri etii yanafichwa,mfano ulishawai
kutaka kuwasimamisha kazi baadhi ya viongozi wako kwa kuwapa barua,sisi kama
wanafunzi hatukupashwa kujua kama umetoa vitisho kwa watu hao sababu
hawakufuata matakwa yako,hii inaonesha ni jinsi gani team yako haina watu
dhabiti kusimamia shughuli za serikali na uongozi kiujumlaa,mh leo unakosa
imani na viongozi uliowateua mwenyewe na kuwaapisha mbele ya kadamnasi kwamba
watalinda na kutetea masrahi ya wanafunzi na serikali yako?huoni unatupa picha
kuwa haukuwa makini wala hukujali masuala ya msingi katika kutengeneza team
work yako?mh:Rais uongozi si kupuliza filimbi,japo hata kupuliza hiyo filimbi
zinahitajika sifa na ujuzi ili uweze kupuliza vizuri.
nashindwa
kuelewa inakuaje viongozi wako leo
wanakusaliti?au kunajambo haliendi sawa?haya ni maswali yangu kwako na serikali
yako kiujumla ,unawezaje kumtoa mbwa
ndani na kumkalibisha chui?hao washauri
wako kweli wanania nzuli na serikali yako?
Tunakumbuka
ahadi zako mh: sijajua mpaka sasa umetekeleza kwa asilimia ngapi sababu hakuna
mawasiliano kati yetu sisi wanafuzi na serikali yako na kama yangekuwepo basi
tungepewa hata feed back juu ya utekelezaji wa ahadi zako kipindi cha kampeni ,si kama sina jicho kuona
mazuli machache yaliyofanywa na serikali yako laaahasha:ila nimekua na jicho
kama lako kututeulia viongozi wasiojua dhamana yao kama viongozi wa serikali ya
wanafunzi.
Siku zote mambo mazuli huigwaaa
napata wakati mgumu sana kuona uongozi ujao utaiga nini na kujifunza nini
kutoka katika serikali yako,serikali yako naifananisha na serikali kuu ya
tanzania
kwani mambo ya akina jairo,luhanjo hayakosekani katika serikali isiyona
udhubutu,si kana kwamba wanafuzi ni wajinga hapana ila wanaitaji busara zako
katika kuiendesha serikali yako,
Katika
serikali yoyote ile fursa zinapopatikana huwa ni kwa maslahi ya wanafuzi wote
na si kwa kundi flani la watu kwa maslahi ya
watu wachache,inakuajee fursa hizo kuwapata viongozi wako tuu au watu
wakaribu na viongozi wako?ikiwa unatambua vizuri slogani yako UNITY FOR CHANGE mh Raisi tunaitaji
mabadiliko.






0 comments:
Post a Comment