Bunge la serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu cha tumaini dar
es salaam TURSODACO limeunda kamati ya uchunguzi kuchunguza ubadhilifu wa pesa
za wanafuunzi katika wizara ya michezo na jamii.
Wabunge walikutana
jana kujadili shtuma zilizoletwa na serikali ya wanafunzi kufuatia matumizi
mabovu ya pesa za wanafunzi zilizo tolewa kwa lengo la kufanyika kwa sherehe za
kuwakalibisaha wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2011.
Wizara husika iliomba zaidi ya milioni tanao katika serikali
ya wanfunzi kwa lengo la kukamilisha na
kufanikisha kwa sherehe hizo.hivyo bunge la wanafuzi lili lidhia bajeti hiyo
kutokana na mahitaji yaliyo bainishwa katika kufanikisha kwa sherehe hiyo na
waziri husika,kwani alidai kungekuwepo na ulinzi kutoka katika makampuni
yanayojishirikisha na ulinzi,ungejengwa uzio kwa lengo la kuzuia wanafunzi
kutoingia baharini usiku,ingejengwa steji,na wanafunzi wangepewa vinywaji kama
soda na maji.
Kwa mujibu wa wanafuzi waliohudhulia sherehe hiyo wanadai
hivyo vitu vyote vilivyoaidiwa havikuwepo,jambo lililosababisha wanafunzi
kutaka kumpiga waziri husika kwani walio9na wamedanganywa,nae makamu wa Raisi
wa Serikali ya wanafunzi mbwayu amekili kwamba ahadi alizotoa waziri wake
hazikutimia,hivyo serikali ilingia wasiwasi wa utendaji wa waziri huyo hivyo
walimuandikia barua kutaka apumzike ili uchunguzi ufanyike.
Waziri husika sulleman adamu aliandika barua kwa serikali ya
wanafunzi kuomba kujiuzulu ili apishe uchunguzi ufanyike juu yake,hivyo kamati
ya jumla ya watu wa tano ikiongozwa na mwenyekiti nyalusi kamati itaanza kazi
rasmi wiki hii na kutoa report siku litapofanyika college baraza.






0 comments:
Post a Comment