Masaa kadha yakiwa
yamesalia kwa vinara wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba kukutana na
Azam FC katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar
es Salaam, makocha wa timu hizo wameshindwa kutambiana.
Imezoeleka kwa kila
Timu zinazoingia Dimbani kupeana vigambo vya hapa na pale kwa
kuoneshana ubavu kabla hata ya kuanza kuchezwa kwa mechi hizo lakini
hali imekuwa tofauti kwa mechi ya Simba na Azam Fc ambao leo
wataingia Dimbani kuchuana
Simba inatarajiwa kushuka uwanjani
kwa tahadhari kubwa, kwani endapo itakubali kipigo itapoteza uongozi
wa ligi hiyo kutokana na kuwa na pointi sawa na Azam lakini vinara
hao wakiizidi kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na
kufungwa.
Kama ilivyo kwa Simba, Azam nayo itahitaji kuibuka
na ushindi ili kukaa kileleni mwa ligi hiyo yenye upinzani mkali
tofauti na msimu uliopita.
Katika msimamo wa ligi hiyo
inayoshirikisha timu 14, Simba, Azam na Mbeya City, zote zina pointi
20, lakini Wekundu wa Msimbazi wapo kileleni kutokana na wastani
mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, wakifuatiwa na
'Wanalambalamba', huku wakali hao wa Mbeya wakishika nafasi ya tatu.







0 comments:
Post a Comment