Wednesday, October 30, 2013

HUKUMU YA BABU SEYA IPO MIKONONI MWA JOPO LA MAJAJI


Hukumu ya Wanamuziki wenye asili ya Congo Babu Seya na Mwanaye ambayo imepitiwa leo imefanyiwa mapitio na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Baada ya kupitia kwa Hukumu hiyo Jopo la majaji wa Rufaa linatarajia kutoa hukumu siku ambayo itapangwa hapo baadaye.

Babu seya na Mwanaye walihukumumiwa kifungo cha Maisha baada ya kukutwa na Hatia ya kunajisi na kuwalawiti watoto wadogo.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.



Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia hukumu iliyoitoa mwaka 2010.



0 comments:

Post a Comment