Friday, October 25, 2013

HOMA YA PSQUARE DAR LADYJAYDEE NA MIKE TEE WAFUNGUKA

Zikiwa zimebaki siku Kadhaa kuisha kwa mwezi wa Kumi na kuelekea mwezi wa Kumi na moja Ambapo kutakuwa na Show Kubwa Ya Psquare kutoka Nigeria siku
ya Tarehe 23,wasanii wa Bongo wameanza kufunguka na kuonesha kuwa na shauku kubwa ya kuwashuhudia wakali hao wakifanya yao Tanzania.

Mwanamuziki Mkongwe wa Kike Tanzania ambaye hivi karibuni amejipatia jina Jipya la Annaconda amekili kuwa kwa mwezi huu na huo ujao huenda mwaka mzima kuwa Show hiyo ya Psquare ndiyo Show Kubwa na kali ambayo wanaisubili kwa hamu kwani Kazifananisha show Zingine na Kelele Tu.

"LadyJaydee(Annaconda)Kweli mwezi huu October hakuna show yoyote kubwa ya maana hapa mjini Dar. Makelele tu, show kubwa inapigiwaje PA?? Tunasubiri P Square tu"

Naye mkali wa miondoko ya Hip Hop ambaye amekwisha Hit na Ngoma kibao huku akiwakilisha Mkoa wa Iringa katika Game Mike Tee ambaye kwa sasa anafanya kazi ya muziki na kazi zingine ambazo zinafafa na kipaji chake ukiachilia mbali biashara zake.

Mkali wa Nyaruland amefunguka Mapenzi yake juu ya wakali hao wa Nigeria ambao watatimba Tarehe 23 na kufanya Tamasha kwa masaa mawili mfululizo wakiwa na Band yao.

"Mike Tee (Mnyaru)@PeterPsquare its Mike Tee from Tanzania am the biggest Fan also the Artist am waiting for u guys"

0 comments:

Post a Comment