Wednesday, October 30, 2013

HAMISI KIIZA AMSHIKA SHATI TAMBWE WA SIMBA

Mshambulaiji Mganda Hamisi Kiiza ambaye jana alifunga goli lake la nane katika mechi ya saba aliyocheza msimu huu wakati alipoisaidia timu yake ya Yanga
kuibuka na ushindi wa kujiamini wa magoli 3-0 dhidi ya Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.
 
Kitendo cha Mshambuliaji huyo wa Yanga Kiiza kufikisha Magori Nane amemshika shati mshambuliaji wa Simba Amisi Tambwe ambaye alikuwa akiiongoza kwa kufumania nyavu kwa msimu huu kwa kufumania Nyavu mara Nane akiwa na Simba Sports Club.

Kiiza hakuweza kushiriki mechi nne za awali mwanzo wa Ligi kuu ambapo alikwenda kufanya majaribio Lebanon.

0 comments:

Post a Comment