Umati wa mashabiki
waliojitokeza kwenye tamasha la Kili Music Tour, wakifuatilia onyesho
hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
|
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnum juzi alifanya
kazi kubwa katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye
Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
tamasha
hilo lililohudhuriwa na umati wa mashabiki, waliokuwa wamejawa na
furaha kuwashuhudia wakali wa waliofanya Vizuri katika Muziki kwa
Mwaka 2012.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ akifanya
yake katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika Kigoma.
|
Diamond
alifanya onyesho la aina yake na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa
kelele mno kiasi kwamba kutounesha utaofauti wa kauli kuwa nabii
hakubaliki nyumbani kwani kwake ilikuwa ni Tofauti mno.
Diamond
ambaye alikuwa msanii wa mwisho kupanda kwenye jukwaa, aliwaita
wasanii wenzake ambao ndio wenyeji wa Kigoma kama Recho, Mwasiti
pamoja na Linex na kuimba wimbo wa Leka Dutigite na kuwaamsha
mashabiki waliofurika Uwanjani hapo.
Wasanii
wengine ambao walitumbuiza katika onyesho hilo lenye ujumbe wa
‘Kikwetu Kwetu’ ilikuwa ni pamoja na Lady Jaydee, Barnaba, Ben
Pol, Izzo Bizness, Recho, Prof. J, Fid. Q, Roma, Mwasiti, Linex
pamoja na Kala Jeremiah.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya nchini Izzo Bizness akiwapagawisha
washabiki katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika juzi kwenye
Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
|
0 comments:
Post a Comment