Tuesday, September 3, 2013

BEN PAUL -NITATOA WIMBO MPYA NA KUIBUA KIPAJI KIPYA TAR 8 SEPTEMBER

Msanii wa Bongo Fleva anaetamba na Ngoma ya Jikubali Bernad Paulo alimaarufu kama Ben Paul amedai kuwa tarehe 8 ya Mwezi September antaraji kufanya mambo makubwa matatu katika siku hiyo ambayo ni siku yake ya Kuzaliwa na kutimiza miaka kadhaa katika Ulimwengu huu.
Kwa mujibu wa Ben Paul amesema kuwa Jambo lake la kwanza litakuwa ni Kusherekea Siku ya kuzaliwa ila akadai kwa kuwa anawapenda sana Mashabiki wake hivyo hatajisikia vizuri kusherekea siku yeye na rafiki tu ila amaeamua kushare furaha yake kwa kuwapa Wimbo wake mpya ambao amefanya na mwanadada Alice hivyo atautambulisha katika siku yake ya kuzaliwa.

Jambo la tatu ambalo litafanyika siku hiyohiyo kwa Ben Paul amedai kuwa atakuwa akimtambulisha Mwanamuziki Alice katika Soko la Muziki wa Tanzania na kukuonesha Kipaji hicho kipya katika Masikio ya watanzania kwani anauwezo wa Hali ya Juu ndio maana aliamua kushirikiana nae katika Wimbo wake mpya ambao utakuwa Zawadi kwa Mashabiki wake.

Sept 8 Nitakuwa nasherehekea Vitu vitatu; 1. Kuzaliwa 2. Kutoa wimbo mpya niliomshirikisha Alice 3. Kuibua nyota mpya ya muziki yaani "Alice”

0 comments:

Post a Comment