Mkurungenzi
wa Benki ya CRDB katika tawi la Moshi amebuluzwa mahakamani na
kufunguliwa shitaka la kufanya kosa la Uzalilishaji wa kijinsia dhidi
ya mteja wa benki hiyo ambae amefahamika kwa jina la Lulu Kajembe...!
Mkurugenzi
huyo Bw Francis Mollel alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Mkoa wa Kilimanjaro kwa kosa la kumtukana na kumtolea maneno ya
Kashfa Lulu Kajembe wakati amepanga foleni .
Shauri hilo la jinai namba 365 lilifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo jana chini ya Hakimu Swai.
Mshtakiwa alikana shtaka hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 21, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa.






0 comments:
Post a Comment