NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leo hii ukimuona Paka katulia mahali wakati si kawaida yake, basi ujue hiyo ni dalili ya kuwa hauko mbali na mahali ambapo mpenzi wako huwa anakutania na mpenzi wake mwinngine.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Ikitokea leo wakati wowote ukamwona Panya mweupe amebanisha mahali kwa muda mrefu bila ya kujitingisha, hiyo ni dalili ya kupoteza kitu chako muhimu ambacho kimekusaidia kwa muda mrefu. Mali iliyoibiwa siku nyingi itapatikana.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo hii ukimuona mtu anatafuna kucha , hiyo ni ishara ya kufanikiwa katika mambo yako ya kikazi, adui yako atakuogopa na kukupisha ufanye mambo yako bila ya wasiwasi.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Leo hii ukimuona mtu ana ndevu nyingi nyeupe, basi ujue hiyo ni ishara ya kuwa mambo yako sasa yatafunguka na kukunyookea, ile mikwamo ya hapa na pale itafunguka kwa urahisi.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo katika matembezi yako ukikutana na mwanamme amevaa mkufu wa shanga, hiyo ni dalili ya kupata kila kitu utakachokihitaji bila ya kutumia muda au nguvu nyingi.Unashauriwa kuwa mtu wa ibada na kutoa sadaka.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo Mchana ukikutana na Mwanamme akiwa amevaa Mkufu wa Fedha, hiyo ni dalili ya kutimia kwa ndoto yako ya kupata Mwanamke au Mwanamme mzuri na kutimia kwa Ndoa yako
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Ukimwona mtoto Leo hii pua analia, basi hiyo ni ishara ya wewe kupata mtoto mzuri au utapata mpenzi mpya ambaye utakutana naye bila ya kutegemea. Sherehe utakayohudhuria itakutanisha na wangu wengi ambao hukutegemea.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Ikitokea leo mtu akatema mate mbele yako, basi ujue kuwa ile posa yako imekataliwa. Unahitajika kuwa mkweli kwa kila hatua utakayoichukua.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo hii ukipewa habari kwamba kuna mtu anakuzungumzia, hiyo ni dalili kwamba utakosa yale yote uliyoyategemea na mtu yoyote hawezi kuwekea pingamizi.tegemea kukutana na mtu mkubwa Serikalini ambaye atakusaidia.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Kama Leo hii ukiumwa kichwa au ukikutana na mtu akakuambia anaumwa kichwa, hiyo ni ishara ya kupata habari nzuri. Leo Mkeo au mumeo au mwanao atakuudhi kwa mambo atakayofanya..
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo hii akikujia mtu akataka Msaada wa aina yoyote kutoka kwako, hiyo ni ishara ya kwamba leo utatukuzwa kwa jambo utakalolifanya na utapata matatizo katika malengo yako uliyoyapanga kwa wiki nzima.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo hii Jumatano, Jicho likikucheza au ukikutana na mtu ambaye ameumia Jicho ,basi hiyo ni dalili ya kuwa hutafanikiwa katika mambo ya pesa utakayoyafanya leo.Ili kuepuka hayo jitahidi kumuomba mungu kwa sala.







0 comments:
Post a Comment