Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amedai kuwa amenasa taarifa za siri za kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani.
Profesa
Lipumba alisema hiyo inatokana na wasiwasi kuwa mchakato wa Katiba
Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014 hivyo kutokuwa rahisi kwa
uchaguzi kufanyika mwaka 2015.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la CUF,
Profesa Lipumba alisema kuwa Serikali inataka kuongezewa muda wa
kukaa madarakani kwa miaka miwili ikimaanisha kuwa Serikali ya Awamu
ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete itakaa madarakani hadi mwaka
2017.
Hata
hivyo, madai hayo ya Profesa Lipumba yamepingwa vikali na Serikali na
viongozi wake watatu waandamizi ambapo walijibu walipoulizwa kwa
maandishi na mwandishi wetu mjini Dodoma wanakohudhuria kikao cha
Bunge.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alijibu: “Mchakato wa Katiba
upo ‘on track’ (unakwenda vizuri) hatuna sababu ya kufanya
hivyo.”
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alijibu” “Njooni ofisini
kwangu nitasema ni kitu gani.”
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi
alijibu kwa utani bila ya kufafanua: “Njooni niwajuze, unajua kamba
haitoki Ukambani kama ilivyo kamba.”
Profesa
Lipumba amemwomba Rais Kikwete asilikubali wazo hilo akisema wananchi
hawatakubali na taifa linaweza kuingia katika mtafaruku.
“Nitapenda
kuona Rais Kikwete akikataa jambo hilo kwani litachafua taswira ya
nchi. Hatua hii ni kinyume cha utawala bora,” alisema Profesa
Lipumba.
Alisema
Serikali haipaswi kuhofia uchaguzi kwa sababu ya Katiba kwani bado
uwezekano wa kuandaa uchaguzi wa haki na huru unawezekana kwa
utaratibu mwingine
“Mchakato
wa Katiba unaendelea, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatuambia kwamba
mwaka 2014 tutakuwa na Katiba Mpya, sasa CUF tunasema kwamba hata
kama Katiba Mpya haitapatikana kwa kipindi hicho kuwe na Tume huru ya
Uchaguzi,” alisema Profesa Lipumba.
Source
Mwananchi







0 comments:
Post a Comment