Msanii
Mb Doggy alietamba katika miaka ya 2001 na ngoma kibao kali zikiwemo
Latifa,Siunajua na ngoma zingine kibao na kupotea katika tasnia ya
bongo fleva baada ya kuingia kufanya biashara zake mwenyewe za
vinyago amerudi tena kwenye game ya bongo fleva na makali ya miaka
ile.
Katika
siku za hivi karibuni i Mb Doggy aliamua kuludu katika kazi yake ya
muziki iliyompa jina mjini na mafanikio kadhaa na kuamua kufungua
studio ya kwakwe mwenyewe ilikwenda kwa jina la Makopa japo
hatukusikia kazi yoyote kutoka katika studio yake hiyo lakini sasa
ameachia kibao kipya kinachokwenda kwa jina la MA-DIGINA .
Katika
Joint hii mpya ya MB Doggy ameonesha ukari wake wa kuimba na kucheza
na sauti nzuri na maneno yenye ladha ya kusikilizika kama ambavyo
alikuwa akifahamika katika ngoma zake zote alizofanya poa miaka ya
nyuma.
“mapenzi
ya vita unahasira jawabu hasara wengi wao unawakuta wanaumia hawana
subira”ni moja ya mistari iliyomo katika wimbo huo







0 comments:
Post a Comment