Wednesday, May 29, 2013

KIFO CHA MANGWEAR NI PIGO KWA TASNIA YA MUZIKI-MADAM RITA PAULSEN




Madam Rita Paulsen ambae ni Chief Judge katika shindano la BSS amesema kifo cha Mwanamuziki Albert Mangwear ambae amefariki jana kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya nchini South Africa ni Pigo katika Tasnia ya Muziki nchini.

Kifo cha Albert Mangwair kimenisikitisha sana. Alikuwa ni rafiki yangu na pia tumeshashirikiana kwenye kazi mbalimbali. Kifo cha Ngwair ni pigo kubwa kwa tasnia ya mziki. Natoa pole kwa familia, rafiki, mashabiki na wadau wote wa hip hop”

Albert Mangwear ni kati ya wasanii wachache wa Hip Hop Nchini walioweza kufanya muziki wa Hip Hop kwa Style ya Pekee na kuweza kuwakilisha vizuri Hip Hop kwa Tanzania,alishafanya ngoma kibao ambazo zitaendelea kuishi katika maisha ya kawaida kutokana na aina ya ujumbe uliopo katika nyimbo hizo.

0 comments:

Post a Comment