Jeshi la
Polisi linamsaka Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa tuhuma za
kuhusika katika vurugu zilizotokea juzi katika chuo cha Uhasibu Mkoani Arusha
(IAA) na kusababisha chuo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana.
Kaimu Kamanda
wa Polisi Mkoani Arusha, Ibrahim Kilongo, aliwaaambia waandishi habari kuwa
jeshi hilo limetoa ilani kwa mbunge huyo kujisalimisha polisi haraka.
Wakati polisi
wakisema hayo, Lema ameeleza kushangazwa na hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha
kutoa amri ya kumkamata.
Alisema kibali
cha kukamatwa kwake ni lazima kitoke kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Lema aliyasema
hayo wakati akizungumza na waandishi jijini hapa na kuwa atakamatwa ikiwa
Spika Makinda atatoa kibali cha kukamatwa kwani yeye ni mbunge halali wa Arusha
Mjini.
Pia aliwapa
pole wanafunzi kwa msiba wa mwanafunzi mwenzao kisha kuwapa pole wanafunzi
wengine waliokumbwa na kadhia ya kupigwa mabomu juzi eneo la chuo wakati
wakidai haki zao za msingi ikiwamo kuhoji matukio ya vifo vya wanafunzi wenzao
vinavyotokea mara kwa mara chuoni hapo.
Hata hivyo,
kamanda Kilongo alisema: “Tunamtaka popote alipo afike mwenyewe polisi na
bado tunaendelea kumtafuta popote alipo, ni muhimu afike tufanye naye mahojiano
kuhusu yaliyotokea katika chuo cha uhasibu."
Lema
anatuhumiwa kuhusika katika vurugu zilizopekea kudhalilishwa na kuzomewa kwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Mara baada ya
kutulizwa kwa vurugu hizo, Mulongo aliliagiza jeshi la polisi kumkamata Mbunge
huyo kwa kile kilicholezwa kuwa ni kumhusisha na vurugu zilizotokea chuoni hapo
juzi.
Katika tukio
hilo lililosababisha mabomu ya machozi kurindima kwa kwa muda chuoni hapo,
Mulongo alijikuta akizomewa baada ya kushindwa kuhutubia mamia ya wanafunzi.
Awali, Naibu Mkuu wa Chuo cha
Uhasibu jijini Arusha, Faraji Kasidi, alisema chuo hicho kimebeba jukumu la
kuusafirisha mwili wa mwanafunzi Henry Kago (22) na kuupeleka nyumbani kwao
Iringa kwa ajili ya mazishi.
CHANZO:
NIPASHE






0 comments:
Post a Comment