![]() |
| mwanaharakati Bw Renatus mkinga akifunguka |
madaktari
wana moyo wa utendaji kazi na kuokoa maisha ya watanzania wanaosumbuliwa na
magonjwa mbalimbali,hili limethibitishwa na mwanaharakati na mtetezi wa
wanyonge BW Renatus MKINGA ,
akiwa
anazungumza na kituo kimoja cha television jijini dare salaam leo asubuhi
mwanaharakati huyo amesema madaktari wanamoyo wa utendaji kazi bali serikali
pamoja na viongozi wamekua chanzo cha matatizo mbalimbali katika hospitali za
hapa nchini,hivyo kuwakatisha tama na moyo katika utendaji wao wa kazi.
‘’Jamani
mimi nililazwa pale MUHIMBILI hivyo nimeshuhudia jinsi madaktari walivyo makini
na kazi yao kwa kuwasaidia wagonjwa ili waludi katika halizao za awali,sema
sasa MUHIMBILI vifaa hakuna,madawa hakuna,mashine za kufua mashuka ni
mbovu,film x ray hakuna jamani katika mazingira hayo sasa madaktari wanafanya
nini? Hili nalo ndilo moja ya vitu vinavyowafanya wagome madkati wetu sababu
anakosa ufanisi wa kazi kutokana na kukosa vitendea kazi,serikali ipo wap?”
Akiongezea ,mkinga
alidai kuwa madaktari wanaingia katika mgomo tena hiyo kesho sababu kubwa
serikali imeshindwa kutekeleza makubaliano yao yakutaka viongozi wajuu katika sekta
ya afya akiwemo waziri wa afya na naibu wake, kuwawajibishwa kutokana na kuleta
mkologano wa mambo.
ni masaa kadhaa yamebakia madaktari kuingia katika mgomo,yaani ni muda mfupi umebakia watanzania tunaanza kupoteza ndugu zetu kwa kukosa huduma pindi wafikishwapo hospitali hii yote ni sababu tu wa watu wachache tuu wenye nia ya mbaya na uroho wa madaraka,
MUNGU IBARIKI TANZANIA,







0 comments:
Post a Comment