Thursday, February 13, 2014

DIAMOND PLATNUM,JOH MAKINI VANESSA KUFANYA SHOW COCO BEACH BURE.

Wasanii wa bongo fleva wanaofanya poa kunako muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na mfalme wa hip hop, Joh Makini watafanya Show kali
kwa vijana katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha na mji wa Moshi kuanzia Jumapili hii.

Maurice Njowoka alisema kuwa kazi hiyo ya kutoa burudani kali kwa vijana itaanza rasmi kwenye fukwe za Coco jijini Dar es Salaam Jumapili huku Diamond na wakali wenzake wakikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa kizazi kipya ambao watapata burudani bure bila ya kulipa viingilio.

"Lengo la burudani hii ni kutoa fursa kwa vijana, hasa ambao wamekuwa wakikosa burudani za aina hii kwa kushindwa kulipia viingilio, kufurahi pamoja na marafiki zao huku wakiburudika na bidhaa zetu," alisema Njowoka huku akiwaomba vijana kujitokeza kwa wingi Dar es Salaam Jumapili na maeneo mengine ambako kampeni hiyo itawezeshwa na kampuni yao.

0 comments:

Post a Comment