Monday, November 4, 2013

TUTAMALIZA LIGI KWA HESHIMA KUBWA-SIMBA SPORT CLUB

Baada ya kuondolewa katika Nafasi ya juu kabisaa Simba Sports Club ambayo kwa sasa inakamatiwa na Azam Fc ikifuatiwa na Mbeya City huku Simba
ikichukua nafasi ya NNE Kocha wa Simba Kibadeni amefunguka na kusema kuwa watamaliza Mzunguko wa kwanza wa Ligi kwa heshima.

Kikosi cha Simba jana jioni kilitarajiwa kuingia kambini Bamba Beach, Kigamboni kwa ajili ya kujiandaa na mechi yake ya kesho dhidi ya Ashanti United.

Kibadeni alisema wachezaji wake wanaendelea vizuri na mazoezi huku kila mmoja akijipanga kucheza kwa juhudi kwa lengo la kupata pointi tatu muhimu.

"Tuko vizuri na tunaamini tutamaliza kwa heshima, msimu huu tulipanga kujenga timu, lakini hapa tulipofika si pabaya, tumefungwa mechi moja tu," Kibadeni alisema.

0 comments:

Post a Comment