Friday, October 4, 2013

MSANII 20% AMALIZA BIFU NA MAN WATER

Msanii aliyevunja rekodi kwa kupata Tuzo nyingi kwa mara moja kwa mwaka 2011-2012 Mpaka sasa Mfalme wa Kimanzichana, Hamis Abbas
Kinzasa ‘20%’ ameamua kurudi na kumaliza tofauti yao kati yake na Produza aliyetengeneza Ngoma nyingi zilizomuweka kileleni Mkali huyo ambaye anafahamika kwa jina la Man Water.

Toka walipotofautiana na Mtayarishaji huyo Msanii 20% hajawahi kufanya kazi ambayo ilifanikiwa kumrudisha tena katika Ramani ya muziki na kuwashika Mashabiki kama ilivyokuwa awali.

Lakini tunaamini kuwa Msanii huyo amejifunza jambo hivyo hatutegemei kusikia suala kama hilo limejirudia tena kwa wawili hao kuingia katika tofauti kwa kosa ambalo lilijitokeza mwanzo.

Niwatakieni mafanikio mema na imani yangu ni kubwa kuwa Man Water atafanya kazi ya kumrudisha Msanii 20% kwani hata mtoto akichafua kiganja chako unachofanya ni kusafisha na maisha yanaendelea na si kukata kiganja.

0 comments:

Post a Comment