Winga wa Yanga na timu
ya Taifa Mrisho Ngasa amefunguka na kusema kuwa ushirikiano mzuri
wanaouonyesha wakiwa uwanjani kicheza sambamba na Hamisi
Kiiza,
umepeleke wao kuunda Bendi yao inayokwenda kwa jina la 'Danger Zone'.
Kwa sasa tuna
'kombinesheni' (muunganiko) kali kwenye safu yetu ya ushambuliaji
ambayo tumeamua kuiita Bendi ya 'Danger Zone' kwa sababu mimi na
Kiiza tunapokuwa kwenye eneo la hatari muda wowote tunafanya
maajabu," alifafanua Ngasa.
Ngasa ambaye ameifungia Yanga
mabao matatu katika mechi tano alizocheza msimu huu tangu atoke
kifungoni huku akitoa pasi tano za mwisho, anaamini kujituma kwake
mazoezini na kwenye mechi ndiko kunakomfanya ang'are katika kikosi
cha klabu yake msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
"Namshukuru
Mungu kwa kunisaidia kufanya vizuri licha ya kuandamwa na jambo zito
la kusimamishwa kucheza mwanzoni mwa ligi na kulipa mamilioni ya
shilingi.
(Nukuu zote
chanzo:Nipashe)







0 comments:
Post a Comment