Malengo ni jambo
moja kubwa na jambo la msingi sanaa ambalo binadamu wote tunapaswa
kujiwekea na kusimamia ili yatimiye.Nakumbuka siku ya
kwanza...!
nafanya Interview na Produza Sheddy Clever akiwa katika studio
yake pande za Tabata aliniambia Moja ya ndoto zake nikuona anafanya
Wimbo Mzuri na Diamond Platnum siku moja.
Baada ya muda
kupita nilisikia kuwa ameanza kufanya kazi na Msanii ambae alikuwa
akiwaza siku moja kufanya nae kazi, hatimae lengo lake limeweza
kutimia kwani amefanikiwa kufanya kazi nzuri ambayo inazungumziwa na
watu wengi na kuhusishwa na kuibiwa kwa Beat.
Nijuacho mimi
katika Wimbo wa My Number One Msanii pamoja na Produza wameshirikiana
vizuri kutengeneza kitu kizuri,Suala la Beat ilikuwa ya Dayna au
sijui ilikuwa ya Nani sio hoja ya kusimamia kwani miliki ya Muziki ni
ya Produza,kazi ya Msanii ni kuimba,kutunga mashairi,na kutafuta
style nzuri ambayo itabamba watu na kazi ya Produza ni kutengeneza
Muziki.
Inanishangaza
Msanii anaibuka na kusema kuwa Muziki au Beat ni mali yake ,Najiuliza
ni yake kwa misingi ipi?
Nijuacho mimi
Muziki ni mali ya Produza ila kama msanii amebuni Melody,Tone na
style ya uimbaji hivyo ni mali yake yeye pamoja na Mistari iliyopo
katika Wimbo husika.
lakini suala la
Beats au muziki huo ni ubunifu wa Mtu mwingine ambae ni produza,Sasa
iweje Dyana useme Sheddy Clever ameuza beat yako kwa Diamond?Je!
Sikiuzi wewe ni Produza wa Muziki kwamba ulikaa ukaumiza kichwa chako
na nguvu yako kutengeneza huo muziki?
Mimi naamini kuwa
Muziki ni mali ya Produza kwakuwa ametumia ubunifu wake na akili yake
kutengeneza huo mdundo ambao wewe unasema wa kwako.
Na wewe ulifanya
kazi yako ya kubuni Melody na Tone ya Wimbo wako ili mwisho wa siku
ngoma iweze kusikika vizuri hivyo leo ungeibuka na kuniambia Diamond
ameiba wimbo wangu kitu cha haraka kusikiliza kwangu mimi ni
Melody,Tone na Style ya Uimbaji zilizotumika katika Nyimbo hizo
pamoja na uandishi maana ndicho unachomiliki Msanii lakini huwezi
sema Diamond Platnum kaiba wimbo wako kisa Beat zinafanana sasa hapo
amekuibia nini?
Katika Nchi za
wenzetu ni Wasanii wachache sanaa ambae anaweza kuingia studio na
kulipa Pesa yake mwenyewe ili akatengenezewa Wimbo na Produza Ndio
maana wengi wao wanaishia kuwa Chini ya Lebo fulani na muziki wa Huyo
Msanii unakuwa chini ya Lebo husika na si mali ya Msaniii.
Kuna kila haja
Wasanii wetu wa Bongo kuitafuta Elimu ya muziki tuufanyao ili
kujiongezea uelewa na maarifa zaidi.







0 comments:
Post a Comment